Mambo Yakienda Vizuri, Patrick Aussems Kocha Mkuu Simba

Mambo Yakienda Vizuri, Patrick Aussems Kocha Mkuu Simba

1
1109
0
Friday, 06 July 2018
Sports
Kama mambo yatakwenda sawa, Kocha Patrick Aussems atasaini mkataba leo kuanza kuinoa Simba.
Aussems raia wa Ubelgiji tayari yuko nchini akiendelea na mazungumzo na Simba.
Jana alikuwa uwanjani kuishuhudia Simba ikiivaa Singida United katika mechi ya michuano ya Kombe la Kagame.

“Kweli kocha yuko nchini na kama mambo yatakwenda vizuri basi atasaini kati ya leo au kesho. Tayari ameiona timu ikicheza dhidi ya Singida United. Amekuwa na maoni yake ingawa hajazungumza sana,” kilieleza chanzo

Aussems mwenye umri wa miaka 51 ni kati ya makocha waliowahi kuzinoa timu mbalimbali za Afrika.
AC Leopards ya Congo, ni moja ya timu ambazo alifanya nazo vizuri kama ilivyokuwa kwa KSA Yaounde ya Cameroon.
Kabla aliwa kuwa kocha msaidizi nchini Ufaransa ambako alizinoa timu za Reims na SCO Angers lakini akafanikiwa kuwa kocha mkuu akiinoa Stade Beaucairois ya Ufaransa pia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *