Zaidi ya watu milioni 820 au 10.8% duniani bado wanakabiliwa na njaa, inasema ripoti ya Umoja wa Mataifa wakati dunia ikiadhimisha siku ya njaa siku ya njaa.
Kiwango cha njaa kimepanda karibu katika maeneo yote ya Afrika, na kulifanya bara la Afrika kuwa kanda yenye idadi kubwa ya watu wenye utapiamlo, kwa takriban asilimia 20, ikifuatiwa na Asia ambako zaidi ya asilimia 12 ya wakazi wa bara hilo wana tatizo hilo.
Asilimia 7 ya watu wa Amerika Kusini na Caribbean pia wameathiriwa na utapiamlo. Kuna watoto zaidi ya milioni 40 wenye uzito wa mwili wa kupindukia duniani ,hili kikiwa ni ongezeko la watoto milioni 10 wenye tatizo hilo tangu mwaka 2000.
Japo idadi ya watoto idadi ya watoto walio chini ya umri wa miaka 5 waliodumaa, imepungua kwa ujumla duniani, bado watoto milioni 149 au asilimia 21.9 ya watoto walio chini ya umri wa miaka 5 wamedumaa. Hata hivyo Afrika bado ina kiwango cha juu kuliko mabara mengine cha watoto waliodumaa katika ukuaji.
Mnamo mwaka 2018, mabara ya Africa na Asia ayalikuwa na kiwango cha tisa kwa kumi cha watoto wote waliodumaa duniani (sawa na asilimia 54.9 kwa Afrika na asilimia 39.5 kwa Asia).
Kiwango hicho kinafanya idadi ya waathiriwa wa ukosefu wa usalama wa chakula kufikia zaidi ya watu bilioni mbili.
Tathmini ya kipekee kuhusu kuongezeka kwa uzito wa mwili inaonyesha kwamba kuna ongezeko la haraka la uzito wa mwili miongoni mwa watoto wa shule na watu wazima katika maeneo yote ya Afrika.
Kulingana na Umoja wa Mataifa watoto wa shule hawali matunda na mboga za kutosha, mara kwa mara hula vyakula vyenye kutia nguvu na joto mwilini , na mara nyingi hula vyakula vinavyotengenezwa haraka kama vile vibanzi na vinywaji vya sukari nyingi kama vile soda, na hawafanyi mazoezi ya mwili.
Mazowea haya mabaya , yanaweza kuwa yanachangia kwa sehemu fulani, kuongezeka kwa uzito wa mwili miongoni mwa watoto wa shule, inasema ripoti.
Tatizo hilo linachangiwa, kwa sehemu moja na kuongezeka kwa masoko ya vyakula vilivyopitia mchakato wa viwandani na upatikanaji wake, pamoja na viwango vya chini vya mazoezi ya mwili.
Kudorola wa chumi za dunia pamoja na kufungwa kwa biashara kuu za dunia kumeelezewa kuchangia kwa ukosefu wa hivi karibuni wa usalama wa chakula pamoja na ukosefu wa virutubisho vya mwili unaoendelea, pamoja na na ukosefu wa sera za muda mfupi na mrefu ambazo ni muhimu katika kulinda usalama wa chakula, iwe nyakati za matatizo ya kiuchumi au katika kuandaa sera hizo.
Mabadiliko ya hali ya hewa pia yamechangia kuathiri kilimo na kusababisha kupungua kwa idadi ya wakulimana shughuli za kilimo . “haya yote yamesababisha mabadiliko ya namna chakula kinavyozalishwa, kugawanywa na kuliwa kote duniani – na kujitokeza kwa changamoto mpya za usalama wa chakula na afya .” wanasema wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa.
Wakizungumza kuhusiana na baa la njaa, wakuu hao wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wameapa kuandaa mikakati ya kukabiliana na baa la njaa duniani.
” Matendo yetu ya kukabilana na hali ya njaa inayotatiza dunia yatakuwa thabiti,” Walisema viongozi hao wa Umoja wa Maraifa. na kuongeza kuwa: “Lazima tukabiliane na umaskini na kuandaa muundo wa mikakati ya mabadiliko inayoshirikisha ikiwalenga watu na kushirikisha jamii zilizozo katika hatari ya kuathirika kiuchumi na kujipanga wenyewe ili kumaliza njaa, kuweka usalama wa chakula na kukabiliana na aina zote za utapiamlo.” Wanasema maafisa wa Umoja wa mataifa.
Umoja wa mataifa unasema kuwa kasi ya mafanikio katika kukabiliana na kudumaa kwa mtoto na kupungua kwa idadi ya watoto wachanga wanaozaliwa na uzito wa chini wa mwili ni ya kiwango cha chini sana, na hivyo kupunguza fursa za kufikia mafanikio malengo mengine ya kudumu.
Umoja wa Mataifa unasema kuwa licha ya kwamba kiwango cha kudumaa kwa watoto kimepungua duniani kwa asilimia 10 katika kipindi cha miaka sita, bado mafanikio ni ya taratibu sana kulingana na malengo ya 2030 ambapo kiwango cha watoto wanaodumaa katika ukuaji kinatarajiwa kupunguzwa kwa asilimia 50.