MAMLAKA YA MANUNUZI YA UMMA PPRA YAZIFUNGIA KAMPUNI 7 KUSHIRIKI ZABUNI

MAMLAKA YA MANUNUZI YA UMMA PPRA YAZIFUNGIA KAMPUNI 7 KUSHIRIKI ZABUNI

Like
401
0
Tuesday, 06 October 2015
Local News

MAMLAKA ya Manunuzi ya Umma Tanzania-PPRA-imezifungia kushiriki zabuni kampuni 7 pamoja na wakurugenzi wake kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kampuni hizo kufanya vitendo vya udanganyifu katika manunuzi.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam leo Mwenyekiti wa Bodi wa PPRA Martin Lumbanga amesema kuwa miongoni mwa kampuni hizo kampuni 6 zimefungiwa kwa kipindi cha miaka miwili kwa kukiuka masharti ya mkataba na kampuni moja imefungiwa kwa kosa la kuwasilisha dhamana za zabuni za kughushi.

Miongoni mwa kampuni zilizofungiwa kushiriki kununua zabuni ni pamoja na Pema Tech Company Limited, Nyakire Investment Limited, na General Trading Limited.

Comments are closed.