MANCHESTER CITY YAAGA MICHUANO YA MABINGWA

MANCHESTER CITY YAAGA MICHUANO YA MABINGWA

Like
427
0
Thursday, 19 March 2015
Slider

Manchester  City jana imetolewa kwenye ligi ya mabingwa barani Ulaya na kuwa timu ya mwisho kutoka ligi ya Uingereza kuyaaga mashindano hayo

Kwa matokeo hayo ya jana yanaandika historia nyingine kwakuwa ligi ya Uingereza kushindwa kuingiza timu katika hatua hiyo ikiwa ni mara ya pili katika misimu mitatu.

Katika mchezo uliochezwa jana huko Hispania klabu ya Barcelona ilikuwa mwenyeji wa klabu ya Uingereza Man City katika uwanja wa Nou Camp na mechi hiyo kumalizika kwa Barcelana kuongoza kwa bao moja

Bao la Barcelona lilifungwa na Ivan Rakitic mnamo dakika ya 31 kutoka kwenye pasi nzuri ya Leonel Mess.

Kwa matokeo hayo ya jana yanafanya kuwe na jumla ya magoli kuwa 3-1 na hii ni baada ya Man city kuruhusu kichapo cha magoli 2-1 katika uwanja wa nyumbani.

BARC2 BAR

Comments are closed.