MAOFISA WA POLISI WASHAMBULIWA FERGUSON

MAOFISA WA POLISI WASHAMBULIWA FERGUSON

Like
315
0
Thursday, 12 March 2015
Global News

MAAFISA Polisi wawili wameshambuliwa kwa risasi mjini Ferguson, mji ambao umekuwa katika hali ya wasiwasi mwingi tangu kijana mweusi alipouawa na askari wa kizungu mwezi Agosti.

Afisa mmoja alipigwa usoni mwingine alijeruhiwa begani.Polisi wanasema wote wanapata matibabu hospitalini.

Shambulio la risasi lilitokea nje ya jengo la idara ya Polisi, ambako waandamanaji kadhaa walikusanyika baada ya Mkuu wa Polisi mjini humo Thomas Jackson alipotangaza kujiuzulu.

 

Comments are closed.