MAPATO NA MATUMIZI TFF HADHARANI

MAPATO NA MATUMIZI TFF HADHARANI

Like
609
0
Monday, 19 March 2018
Sports

Rais wa shirikisho la soko tanzania.(TFF)

 

Rais wa shirikisho la miguu tanzania(TFF), WALLACE KARIA ameongea na waandishi wa habari za michezo, Leo hii jiji dar es salaam na kuwaeleza mambo yanayo endelea kwenye shirikisho hilo

MAPATO

Katika kipindi cha miezi Saba(7),Shirikisho limefanikiwa kukusanya kiasi cha Tzs 3,670,397,199.00 kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali  ambavyo ni pamoja na mapato kutoka kwa wadhamini Tzs 2,295,472,151sawa na 62.5% ya mapato yote, makusanyo ya viingilio uwanjani Tzs 378,139,866 sawa na 10.3%. 27.2% ilitokana na Fedha kutoka CAF na FIFA.

MATUMIZI

Katika kipindi hiki Shirikisho lilitumia kiasi cha Tzs 3,752,001,171.00. Sehemu kubwa ya matumizi yalielekezwa kwenye usimamizi wa ligi mbalimbali pamoja na kuandaa timu za taifa ambapo jumla ya Tzs 2,409,150,732 sawa na 64% ya matumizi yote zilitumika.

Asilimia 36 ya Fedha zilizobaki ilitumika kulipia madeni ya Taasisi, Kulipa mishahara ya wafanyakazi, kusaidia mikoa katika maeneo ya miundo mbinu, kuwajengea uwezo wafanyakazi pamoja na kuendesha mafunzo mbalimbali.

Kama Rais wa TFF sijapokea HOJA wala USHAURI wala MAPENDEKEZO yoyote kutoka kwa Wajumbe wangu katika Ngazi zote kuhusiana na Matumizi ya Taasisi, Nasikitika kama kuna anayedai amehoji sijui wapi kwa kuwa kama Rais sijapokea hoja yoyote wala kuwasilishwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji iliyopita ambayo Taarifa ya Kamati ya Fedha iliwasilishwa nakupokelewa na kupitishwa na Kamati ya Utendaji.

MADENI

Katika kipindi hiki,Shirikisho lilianza zoezi la kutathmini madeni iliyoyarithi kutoka kwenye Uongozi uliopita, ambapo deni hilo linafikia Tzs 2,172,000,000 linalodaiwa na watoa huduma mbalimbali, wafanyakazi,wachezaji na makocha.

Asilimia kubwa ya deni hili lilitokana na malimbikizo ya deni la TRA, Workers Compensation Fund na NSSF ambalo lililimbikizwa kwa zaidi ya miaka miwili.

Shirikisho lilifanikiwa kulipa deni lote la michango ya wafanyakazi NSSF jumla ya Tzs 88,000,000 zilizokuwa hazijalipwa kipindi cha miaka miwili, na lilifanya majadiliano na Mamlaka ya Mapato Tanzania kuhusu ulipaji deni la kodi linalofikia Tzs 1,077,000,000, ambapo jumla ya Tzs 315,000,000 zimelipwa na kiasi kilichobaki tumekubaliana kitalipwa kwa awamu kadhaa mpaka deni lote litakapomalizika.

Pia shirikisho limefanikiwa kupunguza mishahara kwa wafanyakazi kutoka Tzs   85,063,092.00 mpaka kufikia 50,000,000.00 baada ya kupunguza idadi ya wafanyakazi kutoka 44 mpaka 21.

Baada ya kuingia madarakani tulifanya majadiliano na makocha wa timu za Taifa kuhusu uhalisia wa malipo yao na kufanikiwa kuokoa zaidi ya dola laki mbili(USD 200,000) kwenye mikataba yao na fedha zilizookolewa zitasaidia shughuli nyingine za mpira wa miguu.

UFUNDI

  1. Kliniki iliyoendeshwa na Kocha PiaSundhage kutoka Sweden
  2. Kozi ya ngazi ya awali ya makocha wa mpira wa miguu

ilifanyika katika mikoa ya Kigoma,Songwe, Lindi, Morogoro na Pwani

  1. Kozi ya ngazi ya kati ya makocha wa mpira wa miguu

Ilifanyika katika mikoa ya Kigoma mara mbili, Manyara na Morogoro.

4.Grassroot & Live your goal project

Kozi hii ilifanyika katika mikoa ya Lindi ambapo washiriki walitoka katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

Pia kozi nyingine ilifanyika katika mkoa wa Mbeya ambapo washiriki walikuwa ni kutoka katika mikoa ya Mbeya, Njombe, Katavi, Songwe na Rukwa

Aidha hii kozi ilifanyika Kigoma na kushirikisha washiriki wa mikoa ya Kigoma na Tabora.

5.Mafunzo ya awali ya Utawala mikoani

Kuna kozi ya utawala na masoko iliyofanyika Dar es Salaam ili kuwaongezea watu wa masoko uwezo wa kuwavutia wadhamini.

6.Mafunzo ya waamuzi

Mafunzo ya waamuzi wa FIFA na Waamuzi wa ngazi ya juu yalifanyika mara tatu jijini Dar es Salaam.

  1. Kozi ya kupandisha daraja kwa Waamuzi

Kozi hii ilifanyika mara mbili katika mikoa ya Dar es Salaam na Mwanza.

  1. Ziara za Mafunzo na kubadilishana uzoefu

Zilifanyika ziara mbalimbali za Waamuzi wetu za kubadilishana uzoefu katika nchi mbalimbali.

  1. Mpango wa ugawaji wa vifaa vya vijana na mafunzo

Tulipoingia madarakani tulikuta uongozi uliopita wameshanunua mipira na imekaa stoo, katika kutekeleza azma ya maendeleo ya vijana ili tuwe na timu za Taifa imara Shirikisho limegawa mipira (100 kwa kila Mkoa) saizi 4 na 3 kwa Mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar, Mikoa imepewa vifaa vya kufundishia (cones and markers) ili vijana wapate fursa ya kuonesha na kuendeleza vipaji vyao kwa maslahi ya Mpira hapa nchini.

Uzinduzi wa zoezi hili ambalo linategemewa kuwa endelevu lilifanyika Uwanja wa Taifa Agosti 3, 2017.

Rais wa TFF aliwakabidhi wajumbe wa Kamati ya Utendaji kwa niaba ya Mikoa yao kwenye Kanda husika, Kwa upande wa Zanzibar Katibu Mkuu wa ZFA alikabidhiwa mipira hiyo kwa ajili ya Mikoa ya Zanzibar.

MASOKO NA HABARI

Tumeendelea kuongeza wadhamini katika maeneo mbalimbali ili kuhakikisha Taasisi inanufaika na bidhaa zake.Lakini pia tumeendelea kuimarisha idara ya habari kwa kuwanunulia nyezo za kufanyia kazi.

UTAWALA BORA

Katika kipindi hiki cha Miezi saba nimesimamia eneo hili kwa uadilifu mkubwa, Kamati zimekuwa zinakutana kabla ya vikao vya Kamati ya Utendaji ili kuhakikisha kila mmoja anashirikishwa.

Mfano, Wakati nilipokuwa mwenyekiti wa Kamati ya Fedha,kwa miaka 4 nilikaa kikao kimoja cha Kamati ya Fedha,Katika Utawala wangu aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ndani ya miezi saba ameitisha vikao visivyopungua vitano.

Nilimuagiza Kaimu Katibu Mkuu kuhakikisha kila Kamati ya Fedha inapohitaji kukutana ahakikishe inakutana na Mtendaji Mkuu amekuwa anatekeleza.

Na kwa sababu nafasi ya Makamu wa Raisi Kikatiba ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Mipango, basi hata mazungumzo ya Mkataba wa Udhamini wa Ligi Kuu msimu 2018/2019 yeye ndiye aliyekuwa anasimamia.

Nimekuwa nafanya hivi ili Taasisi iendeshwe kwa uwazi na kushirikisha kila mmoja,Na nimeendelea kusisitiza kuwa mapato ya matumizi ya Taasisi yatatolewa kwenye vyombo vya Habari ili yawe wazi kwa umma.

SEKRETARIETI YA TFF

Toka tuanze kuunda sekretarieti tumeajiri Wakurugenzi Watatu na Meneja mmoja na wote hawa waliajiriwa na Kamati ya Utendaji, Ofisi ya Katibu Mkuu haijawahi kuajiri mfanyakazi hata mmoja kufikia sasa.

Nafasi ambayo haijajazwa ni nafasi ya Katibu Mkuu ambako Ndugu Kidao Wilfred bado anakaimu.

Kwanza nikiri kazi nzuri inayofanywa na mtendaji mkuu aliyekuwepo katika kuhakikisha Taasisi inapiga hatua kwa kasi kila ninapokutana na watendaji wakuu wa FIFA, CAF na CECAFA wamekuwa hawasiti kunimwagia sifa kwa kuwa na sekretarieti mahiri iliyobadilika katika kufanyia kazi changamoto za Taasisi.

Raisi wa FIFA alisema anaona mabadiliko makubwa ya hatua tunazochukuwa, Lakini Katibu Mkuu wa FIFA alisema nina Sekretarieti ya Vijana wenye hali, nguvu na maono ya kuipeleka Taasisi mbele huo ndio ujumbe wao.

Nimeyasema haya kuwahakikishia nikiwa msimamizi wa sekretarieti, mambo yote ambayo Kaimu Katibu Mkuu amekuwa akiyafanya ni maelekezo yangu au utekelezaji wa maamuzi halali ya kamati ya Utendaji, Kwahiyo nichukuwe fursa hii kupongeza kasi ya sekretarieti katika kusimamia mambo mbalimbali.

Comments are closed.