‘Marekani ikitengeneza makombora sisi pia tutatengeneza’ aonya rais Putin

‘Marekani ikitengeneza makombora sisi pia tutatengeneza’ aonya rais Putin

Like
631
0
Thursday, 06 December 2018
Global News

Urusi itaunda makombora yaliyopigwa marufuku chini ya mkataba wa vita baridi ikiwa Marekani itajiondoa katika mkataba unaodhibiti silaha hizo, ameonya rais Vladimir Putin.

Rais wa Putin anasema tuhuma za Nato dhidi ya taifa lake ni kisingizio cha Marekani kujiondoa katika mkataba

Tamko lake linakuja baada ya shirika la kujihami kwa mataifa ya magharibi Nato, kuilaumu Urusi kwa kukiuka mkataba wa makubaliano kudhibiti uundaji wa makombora ya masafa ya kadri (INF).

Makubaliano hayo yaliyotiwa saini mwaka 1987 kati ya Marekani na USSR,yalipiga marufuku mataifa hayo yote mawili dhidi ya kuunda makombora ya masafa mafupi na yale kadri.

Rais wa Putin amesema tuhuma za Nato dhidi ya taifa lake ni kisingizio cha Marekani kujiondoa katika mkataba huo.

Katika tamko hilo lililoangaziwa kwenye televisheni, kiongozi huyo alisema mataifa mengi yanaunda silaha zilizopigwa marufuku katika mkataba wa INF

“Sasa inaonekana kuwa washirika wetu Marekani wanahisi kwamba mambo yamebadilika sana kiasi cha kuwa wanaonelea ni lazima wao pia wawe na silaha ,” alisema.

“Jibu letu ni nini? Bila shaka – sisi pia tutafuata mkondo huo.”

Rais Donald Trump wa Marekani

Rais wa Marekani Donald Trump siku za hivi karibuni aligusia kuwa taifa hilo huenda likajiondoa katika mkataba huo kutokana na mienendo ya Urusi.

Wadadisi wanasema Urusi unachukulia suala la uundaji wa silaha hizo kama mbinu mbadala ya kuimarisha vikosi vyake na gharama yake ni nafuu.

Alipowasili kwa mazungumzo na mawaziri wa mambo ya nje wa EU, Kiongozi wa muungano wa Ulaya anayesimamia sera za nje Federica Mogherini ametoa wito kwa mataifa hayo mawili kudumisha mkataba huo akiongeza kuwa “Umekuwa hakikisho la amani na usalama barani Ulaya kw amiaka 30 sasa”.

Nato imesema nini?

Siku ya Jumanne, shirika la Nato liliikosoa rasmi Urusi kwa kukiuka kanuni zinazoongoza mkataba huo.

Katika taarifa shirika hilo lilisema: “Washirika wa wote wamekubaliana kuwa Urusi iliunda kombora aina ya ,9M729 ambayo inakiuka mkataba wa INF katika hatia ambayo inatishia usalama wa muungano wa Euro-Atlantic”.

Taarifa hiyo pia ilisema kuwa nchi wanachama wa muungano huo”zinaunga mkono” madai ya Marekani kwamba Urusi ilikiuka mkataba huo, na kuitaka Moscow “kuchukua jukumu la kuutekeleza kikamili”.

Urusi ilirusha kombora katika mazoezi ya kijeshi

Akizungumza baada ya kutolewa kwa taarifa hiyo, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo amesem,a Urusi ina siku 60 ya kurejelea makubaliano hayo ili kutoa nafasi kwa Marekani kusitisha utekelezaji wake.

“Katika kipindi hicho cha siku 60 hatutafanyia majaribio silaha zetu, kuunda au kutumia mfumo wowote , ili kuba nini kitakachofanyika katika kipindi hiyo” alisema.

Urusi imekuwa ikikanusha tuhuma za kukiuka mkataba wa vita baridi.

Mwaka 2014,aliyekuwa rais wa Marekani wakati huo Barak Obama aliishtumu Urusi kwa kukiuka mkataba wa INF, kufuatia madai kuwa ilifanyia majaribio kombora lake la kulipua meli.

Obama aliripotiwa kudumisha mkataba huo kufuatia ushawishi kutoka kwa viongozi wa bra Ulaya, walisema hatua hiyo huenda akaanzisha tena mashindano ya uundaji silaha.

Mara ya mwisho Marekani ilijiondoa katika mkataba wa silaha ilikuwa mwaka 2002, wakati rais George W Bush alipojiondoa kutoka mkataba wa kudhibiti uundaji wa makombora ya nuklia ambayo ilipiga marufuku uundaji wa silaha za kujibu mahambulio ya silaha hizo.

Hatua ya utawala wake wa kuweka kituo cha kujikinga dhidi ya makombora barani ulaya iliikasirisha Kremlin.

Hata hivyo kituo hicho kilifungwa na utawala wa Obama mwaka 2009 na mahala pake pakachukuliwa na mfumo wa ulinzi uliyoimarishwa mwaka 2016.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *