MAREKANI KUIMARISHA USHIRIKIANO NA IRAN

MAREKANI KUIMARISHA USHIRIKIANO NA IRAN

Like
222
0
Friday, 20 March 2015
Global News

RAIS BARRACK OBAMA ametoa ujumbe katika kanda ya video kwa viongozi na raia wa Iran akisema kwamba hapajakuwa na wakati muafaka zaidi katika miongo kadha iliyopita kwa Marekani na Iran kutafuta uhusiano mpya.

Katika ujumbe wa kusherehekea mwaka mpya wa Iran, OBAMA amesema Mataifa hayo mawili yana nafasi ya kihistoria ambayo haipaswi kupotea.

Amesema mazungumzo kuhusu mpango wa nuklia wa Iran yamepiga hatua lakini ameonya kuwa kuna watu wanaopinga mazungumzo juu ya mpango huo kwa nchi zote mbili yaani Marekani na Iran.

Comments are closed.