Marekani kutoa ripoti ya mwisho juu ya mauaji ya Khashoggi

Marekani kutoa ripoti ya mwisho juu ya mauaji ya Khashoggi

Like
594
0
Sunday, 18 November 2018
Global News

Rais Donald Trump amesema jana kwamba Marekani itatoa ripoti yake ya mwisho wiki ijayo juu ya mauaji ya Jamal Khashoggi, kufuatia ripoti ya shirika la ujasusi la nchi hiyo, CIA, iliyosema kwamba Mwanamfalme Mohammed Bin Salman wa Saudi Arabia ndiye aliyeamrisha kuuawa kwa mwandishi habari huyo. Saudi Arabia mara kwa mara imekuwa ikibadilisha kauli yake rasmi juu ya mauaji hayo ya Oktoba 2. Kwanza ilikana kujua chochote kile juu ya mahala alipo Khashoggi na baadaye kusema kwamba aliuawa ndani ya ubalozi wake mdogo wa Istanbul baada ya kuzuka fujo. Akizungumza na waandishi habari, Trump amesema ripoti kamili itatolewa siku mbili zijazo, huenda ikawa Jumatatu au Jumanne. Mauaji hayo yaliyozua ukosoaji wa kimataifa yameharibu uhusiano kati ya Marekani na Saudi Arabia ambayo ni mshirika wake wa muda mrefu. Saudi Arabia ilikataa wito wa kufanyika uchunguzi wa kimataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *