Watu 76 wafa, zaidi ya 1,000 hawajulikani walipo moto wa California

Watu 76 wafa, zaidi ya 1,000 hawajulikani walipo moto wa California

Like
961
0
Sunday, 18 November 2018
Global News
Idadi ya watu wasiojulikana walipo hadi sasa kutokana na moto mbaya kabisa jimbo la California, Marekani, imepindukia 1,200, huku mabaki ya miili 76 ikiwa imepatikana na msako ukiendelea.

Tathmini iliyotolewa na mkuu wa Kaunti ya Butte ulitokea moto huo, Kory Honea, alisema siku ya Jumamosi (Novemba 17) kwamba ongezeko la idadi ya watu wasiojulikana walipo linatokana na juhudi za ofisi yake kuchunguza idadi ya simu za dharura zilizopigwa wakati wa masaa ya awali ya moto huo kuanza mnamo tarehe 8 Novemba.

Timu za uchunguzi ziligundua mabaki ya watu watano zaidi siku ya Jumamosi, na kuifanya idadi ya waliothibitishwa kupoteza maisha hadi sasa kufikia 76, ambapo 63 tayari wameshatambuliwa katika ngazi za awali, wakingojea sasa vipimo vya vinasaba.

Kwa mujibu wa Honea, maafisa wa kaunti hiyo sasa wanapitia orodha ya watu wasiofahamika walipo kwa kulinganisha na wale waliofanikiwa kukimbia, ambapo watu 380 wametambulika walipo na kuondolewa kwenye orodha hiyo tangu Ijumaa.

“Kuna hatua kubwa zimepigwa kwenye hilo, lakinji bado takwimu hizi hazijachambuliwa,” alisema mkuu huyo wa Kanuti ya Butte.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *