MAREKANI NA CUBA KUREJESHA MAHUSIANO YA KIDIPLOMASIA

MAREKANI NA CUBA KUREJESHA MAHUSIANO YA KIDIPLOMASIA

Like
273
0
Thursday, 18 December 2014
Global News

BAADA ya nusu karne ya siasa za Vita Baridi, hatimaye Marekani na Cuba zimetangaza nia ya kurejesha mahusiano ya kidiplomasia.

Hatua hiyo inayochukuliwa kama tukio la kihistoria baina ya mahasimu hao, ilitangazwa jana na Rais Barack Obama wa Marekani, ambaye sasa nchi yake itaacha mtazamo wa kikale ambao kwa miongo kadhaa umeshindwa kuendeleza maslahi ya taifa.

Mjini Havana, Rais Raul Castro wa Cuba naye amelihutubia taifa akisema mataifa hayo mawili yamekubaliana kurejesha mahusiano, hata kama bado tatizo kuu lingalipo. Tangazo hilo liliambatana na mabadilishano ya kimya kimya ya majasusi waliokuwa wamefungwa kwenye nchi hizo, na pia kuachiliwa kwa mfanyakazi wa ujenzi kutoka Marekani,

Comments are closed.