Marekani walaani shambulio la hoteli ya kifahari jijini Nairobi

Marekani walaani shambulio la hoteli ya kifahari jijini Nairobi

Like
585
0
Wednesday, 16 January 2019
Global News

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) Moussa Faki Mahamat amelaani vikali shambulio la Hoteli ya kifahari ya DusitD2 jijini Nairobi.

Katika taarifa yake, Faki amevisifu vyombo vya ulinzi na usalama vya Kenya kwa kuchukua hatua za uokozi wa raia na kupambana na wahalifu mapema iwezekanavyo. Pia amesema tukio hilo linaonesha umuhimu wa kupitia upya mipango ya kuongeza nguvu ya kupambana na vikundi vya kigaidi barani Afrika.

“Mwenyekiti wa Kamisheni anathibitisha utayari wa AU kuendelea kufanya kazi kwa pamoja na Nchi Wanachama katika kupambana na visa vya ugaidi pamoja na harakati za kutuliza hali nchini Somalia na mapambano dhidi ya kundi al-Shabaab kupitia vikosi vyake vya AMISOM.

Balozi wa Marekani anayemaliza muda wake nchini Kenya Bw Robert Godec ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa Marekani inashutumu vikali shambulio hilo.

Amesema maafisa wote wa ubalozi huo wa Marekani wako salama na kwamba Marekani iko tayari kusaidia iwapo usaidizi wake utahitajika.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imethibitisha kuwa raia wake mmoja ni kati ya watu waliopoteza maisha kwenya mkasa huo.

Kuna ripoti kuwa mpaka sasa watu sita wamethibitishwa kupoteza maisha, watanao kwenye mkahawa mmoja ulio ndani ya viunga hivyo na mwengine akipoteza maisha baada ya kufikishwa hospitali.

Bado idadi rasmi ya watu waliofariki haijatolewa na mamlaka husika hata hivyo mfanyakazi mmoja wa jumba la kuhifadhi maiti ameliambia shirika la habari la Reuters kuna miili 15 iliyohifadhiwa kutokana na shambulio hilo.

Kundi la al-Shabab ambalo linadai kutekeleza shambulio hilo limetoa taarifa ya kuwa watu 47 wameuawa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *