Marekani yaweka vikwazo kwa watendaji 15 wa mafuta wa Sudan Kusini

Marekani yaweka vikwazo kwa watendaji 15 wa mafuta wa Sudan Kusini

Like
386
0
Thursday, 22 March 2018
Global News

Marekani Jumatano imeweka vikwazo kwa watendaji 15 wa mafuta wa Sudan Kusini ambao imesema walikuwa vyanzo muhimu cha fedha kwa serikali, hatua ambayo inalenga kuongeza shinikizo kwa rais Salva Kiir kumaliza mgogoro na mzozo wa kibinadamu nchini kwake.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters makampuni na taasisi za serikali huenda katika siku za mbeleni zikahitaji leseni maalum ya kufanya biashara nchini Marekani, wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema.

Serikali ya Sudan Kusini na maafisa ambao ni wala rushwa, wanatumia mapato haya kununua silaha na kufadhili wanamgambo ambao wanadumaza amani, usalama na uthabiti nchini Sudan Kusini taarifa ya wizara ya mambo ya nje imesema. Makundi yaliyo kwenye orodha yalihusika na harakati ambazo ni kinyume na sera za mambo ya nje na maslahi ya Marekani, kwa mujibu wa waraka uliochapishwa na wizara ya biashara ya Marekani Jumatano.

Comments are closed.