WANANCHI KERO MAJI

WANANCHI KERO MAJI

Like
336
0
Thursday, 22 March 2018
Local News

WAKATI TANZANIA LEO INAADHIMISHA SIKU YA MAJI DUNIANI, JIJI LA DSM LIMEKUWA LIKIPOTEZA MAJI ZAIDI YA LITA MILLION 57 AMBAZO ZIMEKUWA ZIKIPOTEA KUPITIA KWA WATU WACHACHE AMBAO WAMEKUWA WAKIHUJUMU NA KUSABABISHA WANANCHI WENGI KUKOSA MAJI.
JOTO TUMEZUNGUMZA NA WAKAZI WA JIJINI DAR ES SALAAM AMBAO WANAELEZA KERO MBALIMBALI WANAZOKUMBANA NAZO JUU YA MAJI SAFI NA SALAMA.

 

KATIKA KUIADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA MAJI DUNIANI KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAJI NA UMWAGILIAJI PROFESA KITILA MKUMBO AMESHIRIKI MKUTANO WA DUNIA WA MAJI AMBAO UNAFANYIKA JIJINI BRASILIA NCHINI BRAZIL.
MKUTANO HUO UMEJADILI MAMBO MBALIMBALI KUHUSU MAENDELEO YA MAJI DUNIANI IKIWA NI PAMOJA NA NAMNA YA KUPATA FEDHA KWA AJILI YA KUWEZESHA MIRADI YA MAJI KATIKA NCHI ZINAZOENDELEA.
PROF MKUMBO ALIKUWA MOJA YA WAZUNGUMZAJI KATIKA MKUTANO HUO NA AMETOA TAMKO KWA NIABA YA SERIKALI, KATIKA KUBORESHA UPATIKANAJI WA MAJI NCHINI NA HII NI PAMOJA NA KUWEKEZA ZAIDI RASILIMALI FEDHA KATIKA SEKTA HIYO.
AMEELEZA KUWA SERIKALI YA TANZANIA IMEWEKA SUALA LA UWEKEZAJI KWENYE SEKTA YA MAJI KUWA NI MOJA YA MAENEO YA VIPAUMBELE NA KUHAKIKISHA IFIKAPO MWAKA 2021 INAKUWA IMEFIKIA MAHITAJI YA MAJI KWA UKARIBU NA KWA UENDELEVU.

Comments are closed.