CHINA imesema mazungumzo baina ya Rais wa nchi hiyo Xi Jinping na Rais wa Marekani Barack Obama yalikuwa yenye manufaa, licha ya kuwa pande hizo mbili hazikuweza kukubaliana juu ya masuala ya udhibiti wa China wa bahari ya China Kusini, pamoja na mpango wa Marekani wa ulinzi wa kutumia makombora dhidi ya Korea Kaskazini.
Wakati wa mazungumzo hayo yaliyofanyika pembezoni mwa mkutano wa kilele juu ya usalama wa silaha za nyuklia, viongozi hao wawili wamekubaliana kuongeza mshikamano utakaohakikisha usalama wa silaha za kinyukilia duniani kote, pamoja na kuongeza jitihada juu ya suala la usalama wa mitandao.