MARIA SHARAPOVA KUIKOSA FED CUP

MARIA SHARAPOVA KUIKOSA FED CUP

Like
229
0
Wednesday, 15 April 2015
Slider

 

Maria Sharapova mchezaji nambari mbili duniani katika mchezo wa tennis hatocheza mchezo wa nusu fainali mwishoni mwa wiki hii dhidi ya mjerumani kwenye mashindano ya Fed Cup yanayofanyika huko Sochi nchini Urusi.

Maamuzi hayo yakumuondoa Sharapova yamekuja kufuatia kusumbuliwa na jeraha la mguu

Akizungumza na waandishi wa habari, Sharapova ameonesha masikitiko yake kutokana na namna alivyokuwa na hamasa ya kufanya vizuri katika mashindano hayo. “ mimi na timu yangu tulibadilisha ratiba ya mazoezi ili kuweza kuiwakilisha nchi yangu katika hatua ya nusu fainali” alisema Sharapova. ” kwa bahati mbaya nimepata jeraha la mguu na haliniruhusu kuwa tayari katika mpambano huu” aliongeza mchezaji huyo.

Comments are closed.