Marlboro mbioni kuhamia kwenye uzalishaji wa bangi

Marlboro mbioni kuhamia kwenye uzalishaji wa bangi

Like
1316
0
Thursday, 06 December 2018
Global News

Kampuni ya Altria, ambayo ni wazalishaji wa chapa maarufu ya sigara za Marlboro wapo katika mazungumzo na kampuni moja ya kuzalisha bangi nchini Canada ili wawekeze mtaji wao.

Kampuni ya Cronos imethibisha kuwa katika mazungumzo na Malboro ambayo inataka kuinunua ili kuingia rasmi kwenye biashara ya bangi.

Canada iliruhusu kisheria uvutaji wa bangi kama starehe mwezi wa Oktoba mwaka huu, ni nchi ya pili kufanya hivyo baada ya Uruguay.

“Tupo kwenye mazungumzo, kampuni ya Altria inataka kuwekeza kwenye kampuni yetu ya Cronos. Bado hatujafikia makubaliano, na hakuna uhakika kwa sasa kama uwekezaji utafanyika,” imesema taarifa ya Cronos.

Tayari makampuni kadhaa duniani yameanza kuweka mipango ya kuwekeza kwenye sekta ya bangi.

Wazalishaji wa bia ya Corona, kampuni ya Constellation Brands imesema itawekeza dola bilioni 4 kwenye kampuni kubwa zaidi ya uzalishaji bangi nchini Cananda, Canopy Growth. Uwekezaji huo ndio mkubwa zaidi mpaka sasa katika biashara ya bangi duniani.

Kampuni maarufu ya vinywaji ya Coca-Cola ni maarufu zaidi kwa kutengeneza soda, lakini sasa inapanga kufanyia majaribio aina mpya ya kinywaji ambacho kitakuwa na bangi.

Kampuni hiyo itashirikiana na kampuni mwenyeji ya kutengeneza bangi iitwayo Aurora Cannabis na lengo kuu la kinywaji hicho litakuwa ni kupunguza maumivu na si kuwalewesha watu.

Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau aliongoza kampeni za kuhalalisha bangi nchini mwake. Hoja yake kuu ilikuwa sheria zilizoharamisha bangi hazikuwa na maana yoyote sababu raia wa nchi hiyo ni miongoni mwa wavutaji wakubwa wa mmea huo.

Matumizi ya bangi yaliharamishwa rasmi mwaka 1923 nchini Canada, lakini kuanzia mwaka 2001 yaliruhusiwa kwa sababu za kimatibabu.

Kuhalalishwa bangi duniani

Katika nchi zote za Afrika Mashariki matumizi ya bangi kwa namna yoyote ile ni marufuku kisheria. Pia ni kosa la jinai kuzalisha na kuuza.

Hata hivyo, kumekuwa na wimbi linalokua kwa kasi la kuruhusu matumizi ya mmea huo.

Lesotho ilikuwa nchi ya kwanza Afrika kuruhusu kilimo na matumizi ya bangi kwa sababu za kiafya tu. Tayari wakulima wamegeukia zao hilo na wanapata pesa maradufu.

Mwezi Aprili mwaka huu, Zimbabwe ilikuwa nchi ya pili Afrika kuhalalisha uzalishaji wa bagi kwa matumizi ya kiafya na kisayansi.

Mahakama hiyo ilifikia uamuzi huo kwa kauli moja, kuruhusu watu wazima kutumia bangi wakiwa majumbani na kukuza kiasi kinachoweza kutosheleza mahitaji binafsi.

Hata hiyyo itakuwa haramua kutumia bangi katika maeneo ya umma au kuiuza.

Mataifa mengi yamehalalisha matumizi ya bangi kwa sababu ya kimatibabu, zikiwemo Marekani, Ujerumani, Italia na Uholanzi.

Nchini Uhispania, inaruhusiwa kukuza bangi kwa matumizi ya bianafsi katika maeneo ya binafsi.

Matumizi ya bangi Uholanzi kimsingi yamebanwa sana. Mtu binafsi anaruhusiwa kuwa na gramu 5 za bangi za matumizi ibansfi ingawa polisi wanaweza kumpokonya mtu bangi hiyo. Matumizi ya bangi yanaruhusiwa katika migahawa maalum.

Je, bangi ni dawa?

Bangi ina kiungo kiitwacho cannabidiol (CBD), ambacho wanasayansi wamekuwa wakichunguza matumizi yake kama dawa.

Tiba za kutumia CBD zimeonyesha mafanikio makubwa katika kupunguza athari za kifafa, hasa kwa watoto.

Majaribio mengi yamefanywa yakiangazia jinsi inaweza kutengenezwa katika viwanda, lakini baadhi ya wazazi wenye watoto wenye kifafa wamekuwa wakinunua mafuta ya bangi yenye CBD na THC.

Kufikia sasa, hakuna ushahidi sana wa kisayansi kuhusu usalama na kufanikiwa kwa mafuta haya kama tiba ya kifafa, ingawa ni kweli huwa yana viungo vilivyobainishwa kusaidia kutibu athari za ugonjwa huo.

Sativex, ambayo ni dawa ya kufukizia yenye bangi, imekuwa ikitumia kwa ushauri wa madaktari kisheria Uingereza tangu 2006.

Hutumiwa kutibu kuganda na kushikamana kwa misuli pamoja na mkazo wa ghafla wa misuli kwa watu wenye ugonjwa wa kukacha kwa seli au tishu kwa Kiingereza multiple sclerosis.

Madaktari wakati mwingine huwashauri wagonjwa kuitumia kwa sababu nyingine, lakini nje ya matumizi yaliyoruhusiwa kisheria.

Kuna dawa nyingine iitwayo Nabilone inaoruhusiwa kutumiwa. Huwa na aina ya kemikali ya THC ya kuundiwa kwenye viwanda na inaweza kuwasaidia wanaougua saratani kupunguza kichefuchefu wakati wanapopokea tibakemikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *