MASHAMBULIZI DHIDI YA HOUTHI YASITISHWA

MASHAMBULIZI DHIDI YA HOUTHI YASITISHWA

Like
187
0
Monday, 27 July 2015
Global News

MAJESHI ya muungano yakiongozwa na jeshi la Saudi Arabia yamesitisha mashambulizi yake ya angani nchini Yemen, baada ya kuanza muafaka wa amani wa kusitisha mapigano.

Muafaka huo umeafikiwa kati ya majeshi hayo na wapiganaji wa Houthi chini ya Umoja wa mataifa, ili kuyaruhusu mashirika ya utoaji misaada kufikisha chakula na dawa kwa watu wanaothirika na mapigano hayo.

Lakini vyanzo vya habari vinasema kumekuwa na mashambulizi makali ya roketi kusini mwa Yemen, hata kabla ya kuanza kwa muda huo wa kusitisha mapigano.

Comments are closed.