MASHIRIKA YA UN KUSAIDIA UJENZI WA MASHIMO YA VYOO KWENYE SHULE 10 MOSHI

MASHIRIKA YA UN KUSAIDIA UJENZI WA MASHIMO YA VYOO KWENYE SHULE 10 MOSHI

Like
380
0
Monday, 24 August 2015
Local News

IMEELEZWA kuwa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, yanatarajia kusaidia kuboresha matundu ya vyoo katika shule 10 zilizopo manispaa ya Moshi na wilaya ya Moshi vijijini.

 

Hayo yamesemwa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo –MASHIRIKA YA UN KUSAIDIA UJENZI WA MASHIMO YA VYOO KWENYE SHULE 10 MOSHIUNDP– nchini Alvaro Rodriguez katika hafla ya kuweka msingi kwa ajili ya ujenzi wa matundu 18 ya vyoo katika shule ya msingi Kiboriloni wilayani humo.

 

Amesema kuwa pamoja na mashirika hayo kusaidia uboreshaji huo kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa, amewataka wanafunzi kukumbuka kutunza mazingira na miili yao kama sehemu ya mazingira hayo.

 

Comments are closed.