MATOKEO YA LIGI KUU TANZANIA BARA

MATOKEO YA LIGI KUU TANZANIA BARA

Like
413
0
Monday, 19 January 2015
Slider

Polisi Moro imeibana Coastal Union kwao Mkwakwani mjini Tanga.

Wageni hao wameikomalia Coastal na kuilazimisha sare ya bila kufungana.

Polisi Moro ilipoteza nafasi mbili za kufunga katika kipindi cha kwanza. Lakini Coastal nayo ilishindwa kufunga katika kipindi cha pili baada ya kupata nafasi zaidi ya mbili.

Hata hivyo, Polisi ilionyesha soka safi la pasi za uhakika na kumiliki mpira muda mwingi licha ya kuwa ugenin

MECHI YA COASTAL UNION DHIDI YA YANGA YAAHIRISHWA

Mechi kati ya Coastal Union dhidi Yanga kwenye Uwanja Mkwakwani imeahirishwa.

Awali mechi hiyo ilikuwa ichezwe Jumatano, lakini sasa imeahirishwa. Hata hivyo bado haijaelezwa mechi hiyo itachezwa lini.Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga amethibitisha hilo.

“Kweli nimepewa taarifa hizo baada ya timu yetu kuwa na wachezaji kwenye kikosi cha Taifa Stars Maboresho, hivyo mechi imeahirishwa,” alisema Sanga.

Kutokana na hali hiyo, Yanga inaendelea na mazoezi kwa ajili ya mechi nyingi dhidi ya timu ngumu ya Polisi Moro, Jumamosi.

MTIBWA YAREJEA KILELENI

Kikosi cha Mtibwa Sugar kimerejea kileleni kikiwa na pointi 17 ikiwa ni baada ya sare ya leo.

Mtibwa imetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Ruvu JKT katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar.

Sare hiyo inaifanya iringane pointi 17 sawa na Azam FC na Ruvu JKT.

Vijana hao wa Mecky Maxime wanakaa kileleni kutokana na kuwa na wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Comments are closed.