MATUMAINI YA RAHEEM STERLING KUBAKI LIVERPOOL YAFIFIA

MATUMAINI YA RAHEEM STERLING KUBAKI LIVERPOOL YAFIFIA

Like
231
0
Thursday, 09 July 2015
Slider

Mshambuliaji wa England Raheem Sterling hakuhudhulia mafunzo na mazoezi siku ya jumatano huku ikiripotiwa kuwa mchezaji huyo amekataa kwenda kwenye tour na timu yake ya Liverpool ambapo klabu hiyo inatarajiwa kwenda Asia na Australia wiki ijayo.

Sterling, 20, ameipigia simu klabu hiyo na kuwaeleza kuwa hajisikii vizuri kiafya, hii ni kwa mujibu wa vyanzo vya habari nchini Uingereza.

Hali hii ya sasa kwa mchezaji huyu na klabu yake inaongeza uvumi juu ya dili mpya iliyowekwa mezani na Manchester City kwakuzingatia mchezaji huyu kuwa kwenye orodha ya nyota bora zinazowindwa zaidi barani Ulaya.

Sterling amekataa kitita cha pound £100 000 kwa wiki dili iliyowekwa mezani na klabu ya Liverpool huku akiwa amebakiza miaka miwili kuitumikia klabu hiyo lakini tayari imeripotiwa kuwa mchezaji huyu amemwambia Meneja wa klabu hiyo Brendan Rodgers kuwa anataka kuondoka

Comments are closed.