Mauaji ya Khashoggi ‘yalipangwa siku kadhaa kabla

Mauaji ya Khashoggi ‘yalipangwa siku kadhaa kabla

Like
1274
0
Tuesday, 23 October 2018
Global News

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan anasema mauaji ya mwanahabari Jamal Khashoggi yalipangwa siku kadhaa kabla ya kutekelezwa.

Erdogan amesema hayo alipokua akiwahutubia wabunge chama tawala nchini Uturuki.

Amesema Uturuki ina ushahidi mkubwa wa kuthibitisha kuwa mauaji ya Khashoggi yalikuwa yamepangwa na kutekelezwa katika ubalozi mdogo wa Saudia mjini Istanbul Oktoba 2.

Picha ya Jamal Khashoggi na Recep Tayyip Erdogan

Erdogan pia anataka washukiwa wafunguliwe mashtaka mjini Istanbul.

Anataka Saudi Arabia kutoa majibu kuhusu ulipo mwili wa Khashoggi na ni nani aliyeamuru oparesheni hiyo.

Ufalme wa Saudia umetoa taarifa ya kutatanisha kuhusiana na kile kele kilichomkuta mwandishi huyo baada ya kusshiilia kwa wiki kadhaa kwamba alikua hai sasa mamlaka imekiri kuwa aliuawa katika opaeshenio ya kikatili.

Tamko la rais Recep Tayyip Erdogan linakuja huku kongamano la waekezaj likianza nchini Saudi Arabia licha ya baadhi ya serikali na viongozi wakuu wa kibiashara wakijiondoa.

Rais Erdogan amethibitisha kuwa watu 18 wamekamatwa nchini Saudi Arabia kutokana na kesi hiyo japo hajatoa maelezo zaidi kuhusiana na ushahidi uliotolewa

Hakuzungumzia rekodi ya sauti au video ambayo imetajwa katika ripoti ya vyombo vya habari baada ya kutoweka kwa mwanahabari Jamal Khashoggi.

Rais Erdogan pia amesema kuwa kundi la watu 15 wanaosadikiwa kuwa raia wa Saudia waliwasili mjini stanbul kwa kutumia ndege tofauti siku kadhaa kabla ya mauaji yake.

Siku moja kabla ya mauaji ya Khashoggi ,baadhi ya watu kutoka kundi hilo walisafiri hadi msitu wa Belgrad, karibu na ubalozi wa Saudia mjini Istanbul.

Amesema maafisa wa polisi wa Uturuki wamekua wakitafuta mwili wa marehemu katika eneo hilo tangu wiki iliyopita.

Pia ameongeza kuwa watu hao waliondoa kamera za usalama kutoka jengo la ubalozi wa Saudia kabla Khashoggi kufika mahali hapo.

Akizungumza na wabunge wa chama tawala cha AK, Bwana Erdogan amesema “Nataka watu 18 waliokamatwa kufunguliwa mashataka mjini Istanbul.”

Aidha amesema wale wote waliyohusika na mauaji hayo waachukuliwa hatua.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *