Mavugo Afunguka Mstakabali wake na Klabu ya Simba

Mavugo Afunguka Mstakabali wake na Klabu ya Simba

Like
1271
0
Wednesday, 13 June 2018
Sports

Mshambuliaji wa Simba, Mrundi Raudit Mavugo ameongea na #SportsHQ, ambapo amefunguka

na kueleza kuwa mkataba wake na klabu yake unamalizika Julai 7 2018.

Wakati mkataba wake ukielekea kumalizika, Mavugo amesema Timu nyingi zinamtaka zikiwemo Yanga Sc, Singida United, Gor mahia, na Fc Leopard  zinazomuwinda hivi sasa kwa ajili ya kukiboresha kikosi chake.

Mbali na kuhusishwa na Simba, Mavugo pia amesema ataendelea kuitumikia klabu hiyo kutokana na namna ilivyomlea tangu ajiunge na wekundu hao wa Msimbazi endapo watamuongezea mkataba mwingine.

Mavugo ameeleza kwa sasa yupo nchini kwao kwa ajili ya kukitumikia kikosi cha timu yake ya taifa katika mashindano ya kufuzu kuelekea AFCON.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *