MCHUJO KWA WALIOTANGAZA NIA KUPITIA CCM KUFANYIKA LEO

MCHUJO KWA WALIOTANGAZA NIA KUPITIA CCM KUFANYIKA LEO

Like
327
0
Thursday, 09 July 2015
Local News

KAMATI Kuu ya chama cha Mapinduzi-CCM, leo inatarajiwa kufanya Zoezi la uchujaji wa majina ya watu waliotangaza nia ya kugombea nafasi ya urais ndani ya Chama hicho ambapo inatarajiwa leo itatoa majina ya wagombea watano.

CCM inatakiwa kupitisha jina moja la mtu atakayepeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa wabunge na rais unaotarajiwa kufanyika tarehe 25 Oktoba mwaka 2015.

Hapo kesho, Halmashauri kuu ya chama itakutana ambapo itachuja majina hayo matano hadi kufikia matatu kupitia mtindo wa kupiga kura na majina hayo matatu ndiyo yatakayokwenda katika Mkutano Mkuu wa Chama ambao ndio utakaochagua jina moja la huyo mgombea urais kwa tiketi ya CCM.

Comments are closed.