Mchumba wa mwandishi Khashoggi akataa mwaliko wa Donald Trump

Mchumba wa mwandishi Khashoggi akataa mwaliko wa Donald Trump

Like
1756
0
Saturday, 27 October 2018
Global News

Mchumba wa mwanahabari wa Saudia aliyeuawa Jamal Khashoggi anasema amesusia mwaliko wa rais wa Marekani Donald Trump katika Ikulu ya White House kwa madai kiongozi huyo wa haijaonesha nia ya kutaka kujua ukweli kuhusu mauaji hayo ya kikatili.

Hatice Cengiz amekiambia kituo kimoja cha Televisheni nchini Uturuki kwamba mwaliko huo unalenga kubadili maoni ya Wamarekani

Khashoggi aliuawa ndani ya ubalozi mdogo wa Saudi Arabia mjini Istanbul wiki tatu zilizopita.

Riyadh imekanusha madai ya kuhusishwa kwa familia ya kifalme katika mauaji hayo na badala yake imelaumu watu iliyowataja kuwa”maajenti wakatili”

Jamal Khashoggi alikua mkosoaji mkubwa wa Ufalme wa Saudi Arabia

Katika mahojiano ya kusikitisha katika televisheni bi Cengiz alielezea jinsi mchumba wake alivyotoweka baada ya kuingia ubalozi wa Saudia mjini Istanbul.

Anasema ”Kama ningelijua maajenti wa Saudia walikua na njama ya kumuangamiza singelimruhusu kuingia humo”

Awali Saudia ilidai kuwa mwanahabari huyo ambaye alikuwa akiishi Marekani alitoka ndani ya ubalozi wake.

Baada ya shinikizo wakasema kuwa aliuawa alipojaribu kupambana na baadaye wakakiri kuwa aliuawa katika opersheni isiyo rasmi na ambayo haikubarikiwa na Bin Salman.

Huku hayo yakijiri mtoto wa kiume wa Jamal Khashoggi, Salah pamoja na familia yake wamewasili Marekani siku chache baada ya kukutana na Mwanamfalme Mohammed Bin Salman

Mwili haujapatikana

Mwili wa mwanahabari huyo mpaka sasa haujapatikana huku mwendesha mashtaka wa Saudi Arabia akisema mauaji ya Khashoggi yalikuwa yamepangwa.

Mapema wiki hii Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, alisema kuwa mauaji ya mwanahabari Jamal Khashoggi yalipangwa siku kadhaa kabla ya kutekelezwa.

Erdogan alisema hayo alipokua akiwahutubia wabunge chama tawala nchini Uturuki.

Alisema Uturuki ina ushahidi mkubwa wa kuthibitisha kuwa mauaji ya Khashoggi yalikuwa yamepangwa na kutekelezwa katika ubalozi mdogo wa Saudia mjini Istanbul Oktoba 2.

Erdogan sasa anataka washukiwa wa mauaji hayo wafunguliwe mashtaka mjini Istanbul Uturuki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *