MECK SADIQ AMTAKA MKUU WA WILAYA YA KINONDONI KUSIMAMIA KATIBA YA NCHI

MECK SADIQ AMTAKA MKUU WA WILAYA YA KINONDONI KUSIMAMIA KATIBA YA NCHI

Like
308
0
Monday, 23 February 2015
Local News

MKUU wa mkoa wa Dar es salaam SAID MECK SADIQ amemtaka mkuu wa wilaya ya Kinondoni PAUL MAKONDA kusimamia vyema katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuleta maendeleo kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Mheshimiwa SADIKI ametoa wito huo leo jijini Dar es salaam wakati akimuapisha rasmi mkuu wa wilaya hiyo ambapo amesema kuwa kusimamia ipasavyo katiba ya nchi ni suala muhimu katika kuhakikisha usawa unapatikana kwa kila mtu.

Mbali na hayo Mkuu huyo wa Mkoa ameeleza kuwa ili Taifa liwe na wananchi wenye maendeleo ni vyema kwa kiongozi yeyote kusimamia haki bila ubaguzi wa kabila, rangi au dini.

Comments are closed.