MECK SADIQ AZINDUA JARIDA LA SAUTI YA SITI

MECK SADIQ AZINDUA JARIDA LA SAUTI YA SITI

Like
342
0
Friday, 07 November 2014
Local News

MKUU wa Mkoa wa Dar es saalam SAID MECK SADIQ leo amezindua rasmi Jarida la Kitabu cha Sauti ya Siti lenye maandishi ya Nukta Nundu lililoandaliwa na Chama cha wanahabari wanawake-TAMWA kwa kushirikiana na Sauti ya wanawake wenye ulemavu-SWAUTA kwa lengo la kuifikia jamii ya watu wasioona.

Akizungumza na wadau mbalimbali Jijini Dar es Salaam, Mkuu huyo wa Mkoa wa Dar es Salaam, ameeleza kuwa jarida hilo litawasaidia wanawake wasioona kuweza kusoma yaliyoandikwa na kutambua haki zao muhimu pamoja na kufahamu mambo mbalimbali yanayotokea katika jamii.

Mbali na hayo SAID MECK SADIQ, amebainisha kuwa kupitia jarida hilo wanawake hao vilevile wataweza kusoma vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia hususani kwa wanawake na watoto na kufahamu mbinu mbalimbali za kupambana na vitendo hivyo.

Comments are closed.