Melania Trump afanyiwa upasuaji wa figo

Melania Trump afanyiwa upasuaji wa figo

Like
416
0
Tuesday, 15 May 2018
Global News

US First Lady Melania Trump during a listening session with students at the White House in Washington, April 9, 2018.

Mama wa Taifa nchini Marekani Melania Trump amefanyiwa upasuaji wa figo.

Ofisi yake ilisema kuwa madaktari walifanya upasuaji huo kwenye hospitali ya Walter Reed National Military Medical Center.

Upasuji huo ulikuwa wenye mafaninikio na hakukuwa na matatizo yoyote kwa mujibu wa msemaji wake.

Bi Trump, 48, anatarajiwa kutumia muda mwingi wiki hii kupata nafuu hospitalini huko Bethesda, Maryland.

Alisema kampeni hiyo ina lengo la kuhakikisha maisha yenye afya na kuzuia dhuluma.

Pia ilitangazwa Jumatatu kuwa aliyekuwa kiongozi wa wengi wa seneti wa chama cha Democratic Harry Reid, 78, alikuwa amefanyiwa upasuaji wa kongosho.

Familia ya Bw Reid ilisema madaktari kwenye hospitali ya Johns Hopkins Hospital huko Baltimore walikuwa na uhakika kuwa upasuaji huo ulikuwa wenye mafanikio na anapata nafuu vizuri.

Madaktari walikuwa wamegundua tatizo mapema wakati wa uchunguzi wa kawaida wa kiafaya, kwa mujibu wa taaarifa.

Seneta wa Republican John MacCain ambaye mwenyewe anaugua saratani ya ubongo ni kati ya wale waliomtumia ujumbe wa heri njema.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *