MENEJA WA ENGLAND AMEAHIRISHA KIKAO BAADA YA WACHEZAJI KUBANWA NA RATIBA

MENEJA WA ENGLAND AMEAHIRISHA KIKAO BAADA YA WACHEZAJI KUBANWA NA RATIBA

Like
280
0
Wednesday, 14 January 2015
Slider

Meneja wa timu ya taifa ya England Roy Hodgson amejikuta akilazimika kufuta ratiba ya kukutana na wachezaji wake na kupata chakula cha usiku pamoja kufuatia ratiba kuwabana wachezaji hao.

Roy Hodgson alikuwa na lengo la kukutana na wachezaji hao mwishoni mwa mwezi wa kwanza ili kuweza kujadili pamoja ikiwemo ushindi dhidi ya Scotland.

Shirikisho la mpira wa miguu nchini humo limeeleza kuwa timu hiyo pia ilikuwa ipo kwenye utayari wa kikao hicho ila kufuatia kile kilichotokea wamejikuta wakiahirisha kukutana na hakuna upande uliopanga siku ya kukutana tena

Comments are closed.