MGONJWA MWENYE SIKU 7 ZA KUISHI AOMBA KUKUTANA NA EMINEM

MGONJWA MWENYE SIKU 7 ZA KUISHI AOMBA KUKUTANA NA EMINEM

Like
661
0
Tuesday, 13 January 2015
Entertanment

 

Eminem richa ya kuwa na itikadi za kuonyesha hali za ukali na utata kwenye maisha yake lakini pia kwa upande mwingine huenda Eminem ni mtu mwenye huruma pia.

Katika kulithibitisha hili rapa huyu alifanya matembezi kwa mmoja wa mashabiki zake ambae anamatatizo ya kansa ya mifupa

 Gage Garmo mwenye umri wa miaka 17 ambae kwa mujibu wa madaktari waliokuwa wakimfanyia matibabu wamemueleza kuwa ana wiki moja tu ya kuishi kutokana na matatizo aliyokuwa nayo kiafya

 Kama siku tatu zilizopita nyuma familia na marafiki zake walianza kufanya kampeni mitandaoni ilipewa jina la #GetGageGarmoToMeetEminem ikiwa na lengo la kumkutanisha Gage Garmo na msanii wake anaempenda zaidi yani Eminem

Kampeni hiyo ilifanikiwa pale ambapo Eminem alimtembelea shabiki huyo kwa siri akiwa na lengo la kutotaka waandishi wa habari kuusika

Eminem alitumia zaidi ya lisaa kukaa na shabiki huyo wakizungumza na kufanya matembezi ya pamoja hali ambayo ilimuweka Gage sawa kiafya wakati huo na hata baada ya Eminem kuondoka

Comments are closed.