MAHAKAMA ya juu zaidi Korea Kaskazini imemhukumu mhubiri kutoka Canada kifungo cha maisha jela na kazi ngumu.
Hyeon Soo Lim, mwenye umri wa maika 60, aliyekamatwa mjini Pyongyang baada ya kuzuru taifa hilo Januari kwa kazi ya kibinadamu amehukumiwa kwa makosa ya “uhalifu dhidi ya dola.”
Bw Lim, ambaye ni kiongozi wa Light Korean Presbyterian Church, anadaiwa kukiri kuhusika katika njama ya kupanga kupindua serikali na kuunda taifa la kidini.