MIRADI YA UMEME KINYEREZI KUKAMILIKA JUNI MWAKA HUU

MIRADI YA UMEME KINYEREZI KUKAMILIKA JUNI MWAKA HUU

Like
337
0
Wednesday, 04 March 2015
Local News

MENEJA Miradi ya Kinyerezi Mhandisi SIMON JILIMA amesema kuwa mtambo wa Kinyerezi 1 unaojengwa na kampuni ya Yakobsen Elektro ya Norway unatarajia kukamilika mapema Juni mwaka huu.

Mhandisi JILIMA ameeleza hayo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini iliyofanya ziara katika Mtambo huo ili kujionea maendeleo ya ujenzi wake.

Kamati hiyo imeanza ziara ya kutembelea Miradi ya umeme iliyopo katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Singida, Arusha na Kilimanjaro pamoja na kuzungumza na wadau wa Madini aina ya Tanzanite katika mkoa wa Manyara.

KA2 KA4

 

Comments are closed.