MITIHANI ya kumaliza Kidato cha Nne, na Maarifa (QT) unaanza leo nchi nzima katika Shule za Sekondari elfu 4,634 na vituo vya Watahiniwa wa kujitegemea 960.
Mitihani hiyo itakayofanyika kwa muda wa siku 26 itakuwa na jumla ya watahiniwa laki 448 elfu na mia 358 waliojisajili kufanya mtihani huo, ambapo kati ya watahiniwa wa Shule ni laki 394, 243 na wa Kujitegemea ni elfu 54, 115.
Kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa NECTA, Dokta Charles Msonde , kati ya watahiniwa wa shule ambao wamesajiliwa, wavulana ni laki 193, 082 sawa na asilimia 48.97 na wasichana ni 201, 161 sawa na asilimia 51.03.