MKURUGENZI MKUU WA MTN AJIUZULU

MKURUGENZI MKUU WA MTN AJIUZULU

Like
401
0
Monday, 09 November 2015
Global News

MKURUGENZI Mkuu wa kampuni ya simu ya MTN amejiuzulu kufuatia kampuni hiyo kutozwa faini kubwa ya dola bilioni 5.2 na Nigeria

Mkuu huyo wa kampuni hiyo kubwa zaidi barani Afrika Sifiso Dabengwa, aliwasilisha barua ya kujiuzulu mara moja kwa maslahi ya wenye hisa na uendelevu wa kampuni hiyo.

Faini hiyo ilitozwa na Tume ya mawasiliano ya Nigeria kufuatia uamuzi wa MTN kukataa kuzima namba za simu ambazo hazijasajiliwa kwa mujibu wa kanuni mpya za Taifa hilo.

 

Comments are closed.