MOISE KATUMBI ANZISHA CHAMA CHAKE CHA SIASA AKIWA AFRIKA KUSINI

MOISE KATUMBI ANZISHA CHAMA CHAKE CHA SIASA AKIWA AFRIKA KUSINI

Like
276
0
Monday, 12 March 2018
Global News

Rais wa klabu ya TP Mazembe ya katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Moise Katumbi amejitosa kwenye ulingo wa siasa, anazindua chama chake akiwa Afrika Kusini.

Katumbi ni kiongozi wa upinzani ambaye yupo uhamishoni kutoka DR Congo baada ya kutengana na Rais Joseph Kabila.

Katumbi ambaye amewahi kuwa Gavana wa jimbo tajiri zaidi nchini humo Katanga alijiuzulu na kumshtumu rais Kabila kwa uongozi duniani.

Moise Katumbi ni kiongozi wa pekee wa upinzani nchini Congo ambaye ana ushawishi mkubwa na ufuasi mkubwa miongoni mwa raia wa Congo na anayetarajiwa kumpa rais Kabila ushindani mkali endapo atawania tena.

Alitangaza kutaka kuwania urais mwaka 2016, kabla ya uchaguzi huo kuahirishwa.

Katumbi aliondoka DRC Mwezi Mei mwaka 2016 na kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya kupata matibabu punde tu aliposhutumiwa kuwaajiri wapiganaji. Baada ya hapo alihukumiwa bila yeye kuwepo kwa kuuza maeneo kinyume cha sheria na kupatiwa kifungo cha miaka 3 jela.

Anakanusha tuhuma hizo na amewahi kusema kuwa bado anataka kuwania urais katika uchaguzi utakaofuata. Bw Katumbi pia ni ya soka maarufu ya TP Mazembe.

Comments are closed.