MOUNRINHO ASHITAKIWA KWA UTOVU WA NIDHAMU

MOUNRINHO ASHITAKIWA KWA UTOVU WA NIDHAMU

Like
158
0
Tuesday, 27 October 2015
Slider

Meneja wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho ameshtakiwa na chama cha mpira wa miguu FA kwa utovu wa nidhamu.

Mourinho ameshitakiwa na Chama hicho cha mpira kutokana na lugha pamoja na tabia kwa ujumla kwenye mchezo kati ya Chelsea na West Ham United ambapo upande wake ulipokea kichapo.

Mourinho alisimamishwa baada ya kumfuata mwamuzi Jon Moss kwenye chumba chake wakati wa mapumziko siku jumamosi.

Klabu zote mbili zimeshitakiwa kwa kushindwa kuwaongoza wachezaji wao na kutakiwa kutoa majibu ifikapo October 29

Chelsea tayari wameingia hasara ya pound 25,000 ikiwa ni faini kutokana na kupokea kadi za adhabu zaidi ya tano kwenye Premier League.

 

 

Comments are closed.