MSD YAENDELEA NA MRADI WA UZALISHAJI DAWA NA VIFAA TIBA

MSD YAENDELEA NA MRADI WA UZALISHAJI DAWA NA VIFAA TIBA

Like
243
0
Tuesday, 23 December 2014
Local News

BOHARI ya dawa ya Taifa –MSD, imesema inaendelea na mradi wa uzalishaji dawa na vifaa tiba nchini kwa ubia na Sekta binafsi ikiwa ni utekelezaji wa mpango wa mkakati wake wa pili wa miaka sita ulioanza mwezi Julai mwaka huu.
Malengo makuu ya mpango huo ni kuimarisha upatikanaji wa dawa na Vifaa tiba nchini ili kuifanya MSD kuwa kituo bora cha usambazaji wa dawa Barani Afrika.
Akizungumza na Wandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam,Kaimu Mkurugenzi wa MSD, Cosmas Mwaifani, amesema kwakuwa uwezeshaji kwenye viwanda vya uzalishaji dawa unahitaji mtaji mkubwa, ndiyo maana wameamua kutumia sera ya ubia ya Sekta ya Umma na Binafsi- PPP.

Comments are closed.