MSHUKIWA WA BRUSSELS ALIUNDA MABOMU YA PARIS

MSHUKIWA WA BRUSSELS ALIUNDA MABOMU YA PARIS

Like
296
0
Thursday, 24 March 2016
Global News

MAAFISA wa Ufaransa na Ubelgiji wanasema mmoja wa walipuaji wa kujitoa mhanga waliotekeleza mashambulio ya Brussels alikuwa mtaalamu wa kutengeneza mabomu.

Wamesema mshukiwa huyo alihusika katika kuunda mabomu yaliyotumiwa kutekeleza mashambulio ya Paris Novemba mwaka jana na kusababisha vifo vya watu 130.

 

Wakizungumza, bila kutaka kunukuliwa, maafisa hao walisema chembe nasaba za DNA za mshukiwa huyo Najim Laachraoui zilipatikana katika mikanda ya kujilipua iliyotumiwa Paris.

Comments are closed.