Msichana kiziwe aliyesikia sauti yake baada ya upasuaji wa ubongo

Msichana kiziwe aliyesikia sauti yake baada ya upasuaji wa ubongo

Like
747
0
Tuesday, 23 April 2019
Global News

Msichana mwenye umri wa miaka saba Leia Armitage amekuwa akiishi katika maisha ya ukimya kutokana na kutosikia katika kipindi cha miaka miwili ya mwanzo ya masha yake , lakini upasuaji wa hivi karibuni wa ubongo na tiba vimeweza kubadili maisha yake na sasa anaweza kusikia sauti zake na hatimae anaweza kusikia sauti za wazazi wake na kuwambia kuwa anawapenda.

“Tuliamboiwa kuwa unaweza kuweka bomu nyuma yake na asingeliweza kabiza kusikia sauti ya mlipuko wake ,” amesema baba yake Leia , Bob, huku akikumbuka namna walivyobaini kuwa mtoto wao mchanga wa kike alikuwa na aina ya nadra kabisa ya ulemavu wa kutosikia.

Leia, ambaye anatoka katik eneo la Dagenham mashariki mwa London, hakuwa na sikio la ndani au mshipa wa kusikia, hii ikimaanisha kuwa mtambo wa kawaida wa kusaidia mlemavu wa kutosikia wala ule wa kupandikiziwa visingemsaidia lolote.

Matokeo yake, hakutarajiwa kuzungumza- licha ya hatari hizo, wazazi wake walimpigania ili awe mmoja wa watoto wa kwanza nchini Uingereza kupewa kifaa kinachopandikizwa ndani ya ubongo kwa njia ya upasuaji mgumu alipokuw ana umri wa miaka miwili.

Taasisi ya upasuaji huo ya nchini Uingereza NHS imeutaja kama “halisi uliobadilisha maisha ” na imesema kuwa itadhamini kifedha utapandikizaji huo kwa watoto wengine wasioweza kusikia wenye hali kama yake.

Inakadiriwa kuwa watoto wapatao 15 kila mwaka watakiuwa wanachunguzwa kwa ajili ya kufanyikwa upasuaji huo na tisa miongoni mwao watakuwa wanajfanyiwa upasuaji huo

Anasikia honi za magari

Bob anasema kuchagua aina hii ya upasuaji wa wa ubongo ulikuwa ni uamuzi mkubwa kwao, lakini ”tulitaka Leia apate fursa hii muhimu maishani mwake “.

yeye na mkewe Alison walitumai kwamba baada ya upasuaji katika hospitali ya wakfu wa Guy’s and St Thomas’ NHS ,ataweza kusikia kama vile honi za magari wakati atakapokuwa akivuka barabara ili kumfanya awe salama katika dunia hii.

Hata hivyo katika kipindi cha miaka mitano baada ya upasuaji, mafanikio ni makubwa zaidi kuliko walivyotarajia .

lianza polepole, Leia alipoanza kugeuza kichwa chake akisikia sauti ya mlango wa treni inapofungwa baada ya kufanyiwa upasuaji .

Hatimae, alianza kuelewa dhana ya sauti huku wazazi wake wakiendelea kurudia rudia maneno, wakimtaka aigize sauti.

Sasa baada ya matamshi mengi na tiba ya lugha, anaweza kutunga sentensi na kuizungumza ,akijaribu kuimba muziki unapopigwa na kusikia sauti kwenye simu

“Tunaweza kumuita kwenye vyiumba vya juu tukiwa vyumba vya chini na akatusikia ,” Alieleza baba yake Bob.

Nakupenda

Lakini ilikuwa ni katika shule , katika darasa la watoto wanaosikia, ambapo Leia anafanya vizuri zaidi, hii ni kutokana na usaidizi wa kutumia alama za lugha na kumpatia muda wa kiujifunza nae peke yakei

” Anaendelea vizuri zaidi na zaidina hayuko nyuma sana ya wenzake wa umri wake kwa mambo mengi ,”anasema Bob

Nyumbani, anapotumia sauti yake ndio jambo linalowaridhisha zaidi wazazi wake zaidi.

“‘Nakupenda baba’ huenda ni kitu kizuri zaidi nilichowahi kusikia akisema ,” anasema Bob

“Ninapomuweka kiytandani sasa anasema ‘usiku mwema mama’, maneno ambayo hatukutarajia kuyasikia kutoka kwake ,” Alison anasema.

Upasuaji huo hufanyika kwa kuweka kifaa moja kwa moja kwenye ubongo kinachosaidia kuamsha njia za usikivu miongoni mwa watoto wanaozaliwabiola neva za kusikia.

Kitengo cha kupaza sauti na utambuzi wake hufahamisha sehemu nyingine ya kichwa na baadae husafirisha sauti hadi kwenye kifaa na hivyo kumuwezesha mtumiaji kusikia.

Uchochezi huu wa nkielektroniki unaweza kutoa hisia , lakini hauwezi kurejesha usikivu wa kawaida.

Hata hivyo Profesa Dan Jiang, daktari wa masikio na Mkurugenzi wa kituo cha upandikizaji wa tiba katika kiliniki ya wakfu wa Guy’s and St Thomas anadsema baadhi ya watoto wanaweza kukuwa kwa kiwango cha matamshi.

“Matokeo ni tofauti. Baadhi watafanya vema kuliko wengine ,” alisema.

“Lazima wajifunze na watoto wadogo hufanya vizuri kwa hiyo tunapenda kuwawekea watoto vifaa vya kusikia mapema iwezekanavyo .”

Watoto walio chini ya umei wa miaka mitano wako katika nafasi nzuri ya kujifunza kitu kipyana kupona kwa matibabu , alisema.

Susan Daniels, Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya taifa ya watoto wasio sikia lisema: “Kila mtoto asiyesikia ni tofauti , na kwa baadhi teknolojia kama ya kifaa cha kushitua ubongo inaweza kuwafaa na kuleta tofauti kubwa katika maisha yao”.

“Kwa usaidizi unaofaa, watoto wasiosikia wanaweza kusikia kama watoto wenzao wasio na ulemavu huu na uwekezaji huu ni hatua nyingine ya kuhakikisha kuwa watoto wasio sikia hawaachwi nyuma katika jamii” amesema Susan Daniels

cc;BBCswahili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *