Mtatiro Ajiondoa CUF, Ajiunga CCM

Mtatiro Ajiondoa CUF, Ajiunga CCM

Like
417
0
Saturday, 11 August 2018
Local News

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha CUF Julius Mtatiro amejivua uanachama wa chama hicho nakujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM huku akisema kuwa huu ni wakati wake wakwenda kutumia vipaji vyake kikamilifu pia kuwa balozi mkubwa wa Rais Magufuli Ndani na nje ya Nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam amesema kuwa ameamua kuchukua uamuzi huo kwa kuwa jukwaa alilokuwa analisimamia katika siasa kwa miaka kumi limeshindwa kumpa nafasi yakuifanyie nchi yake maendeleo.

Katika hatua nyingine baada ya kutangaza nia hiyo Mtatiro ametoa ahadi yakuwatumikia watanzania pamoja na kupambana na umasikini nakuongeza uamuzi alioufanya sio kwaajili yakutafuta cheo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *