MTOTO WA MWEZI MMOJA APIGWA NA MCHI KICHWANI NA BABA YAKE

MTOTO WA MWEZI MMOJA APIGWA NA MCHI KICHWANI NA BABA YAKE

Like
308
0
Monday, 26 January 2015
Local News

MTOTO mwenye umri wa mwezi mmoja amelazwa katika hospital ya  Wilaya ya  Mpwapwa mkoani Dodoma kutokana na kupigwa na Mchi kichwani na Baba yake Mzazi na kusababisha kupasuka fuvu.

Kwa mujibu wa Mganga Mkuu wa Hospital ya Wilaya ya Mpwapwa ya Benjamin Mkapa Dokta SAID MAWJI amesema kuwa mtoto huyo amepokelewa na amelazwa Wodi namba saba huku hali yake ikiwa mbaya.

Amebainisha kuwa wanaendelea kumfanyia uchunguzi hasa katika fuvu la kichwa ambapo uchunguzi wa awali umeonyesha limepasuka kutokana na kupigwa ama kuangukiwa na kitu chenye uzito mkubwa.

 

Comments are closed.