MTU ASIYEFAHAMIKA AINGILIA WANAWAKE KINGUVU NYAKATI ZA USIKU

MTU ASIYEFAHAMIKA AINGILIA WANAWAKE KINGUVU NYAKATI ZA USIKU

Like
342
0
Thursday, 26 May 2016
Local News

WANAWAKE wakazi wa mji wa Kigoma, wamekumbwa na taharuki kufuatia kuibuka mtu asiyefahamika anayewaingilia kinguvu wakati wamelala kwenye nyumba zao usiku huku akitumia panga kuwatisha au kuwakata kata mapanga sehemu mbali mbali za miili yao wale wanaokataa kutekeleza matakwa yake.

 

Mpaka sasa zaidi ya wanawake 10 wanaelezwa kuvamiwa na mtu huyo ambaye kwa sasa ni maarufu kwa jina la Teleza, na inadaiwa kuwa huwafuata Zaidi wanawake wasio na waume na hutumia kisu kuharibu vitasa vya milango kabla ya kuingia ndani.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Ferdinand Mtui, amethibitisha taarifa za matukio hayo huku akieleza kuwa tayari mtu mmoja amekamatwa na anaendelea kuhojiwa.

Comments are closed.