TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
03/09/2015
BAADA ya kumalizika kwa Tamasha la muziki mnene Mtaa kwa Mtaa awamu ya kwanza, (Muziki mnene bango) ambapo mashabiki na wasikilizaji wengi wa EFM wamejishindia zawadi kabambe, Sasa ni zamu ya wapenzi wa burudani na mambo ya party.
Muziki mnene bar kwa bar ni tukio ambalo lina wakutanisha wasikilizaji na mashabiki wa EFM na wakali wa EFM kutoka wilaya za kinondoni, Ilala na Temeke katika mkoa wa Dar er Salaam, na kwa sasa Muziki mnene utapelekwa pia katika mkoa wa Pwani.
Maeneo ambayo wanatakiwa kukaa tayari kwa Muziki mnene bar kwa bar utakaoporomoshwa na Rdjs wakali wa Efm, ni pamoja na Kibaha, Mlandizi, Mkuranga, Bagamoyo, Kisarawe, Kigamboni na maeneo mengine mengi kwa ajili ya kuhakikisha tunakonga nyoyo za mashabiki wetu.
Muziki Mnene bar kwa bar mwaka huu inatarajiwa kuanza rasmi jumamosi hii tarehe 5/09/2015 na moto utawashwa kwa kuanzia Mkuranga ambako mbali na kutoa Burudani, tutaanza na mchezo wa mpira ili kuwapa nafasi wale wasio na uwezo wa kujumuika nasi tuonane nao mchana.
Na kama ilivyokawaida yetu, mwishoni tutakuwa na Tamasha kubwa la hitimisho ambalo litafanyika jijini Dar es salaam ambalo safari hii limeboreshwa na kuongezwa vionjo vingi sana.
“Ninawaomba wasikilizaji wetu wakae mkao wa kula maana tutawafikia na kuwamiminia Burudani ambayo pia itarushwa live kutoka eneo husika kupitia kituo chao cha 93.7 EFM. Njoo tuonane, tufahamiane na tuijenge Radio yetu efm ambayo kwetu Muziki unaongea”.
Muziki mnene awamu hii tunawadhamini ambao pia naomba niwatambulishe kwenu na kuwashukuru ambao ni kampuni ya simu mpya kabisa hapa Tanzania ya Smart, kampuni ambayo huduma zake ni za gharama ndogo zaidi,
Kwahiyo mwaka huu Smart watakuwa na sisi katika kuupeleka Muziki Mnene bar kwa bar kwa mashabiki wa EFM.
Mwisho niwashukuru sana kwa mwitikio wenu na kwakuwa tumeendelea kushirikiana mara nyingi hivyo naomba tuendelee kushirikiana. Asanteni sana kwakunisikiliza.
IMETOLEWA NA
DENIS SSEBO
MENEJA WA MAWASILIANO – EFM.
picha kushoto ni Dennis Ssebo Meneja mahusiano efm