MVUA YA MAWE YALETA KIZAAZAA BUNDA

MVUA YA MAWE YALETA KIZAAZAA BUNDA

Like
411
0
Friday, 14 November 2014
Local News

MVUA kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo mkali imenyesha na kusababisha maafa katika Wilaya ya Bunda mkoani Mara ikiwa ni pamoja na watoto wawili kujeruhiwa na mmoja kuvunjika mkono kutokana na kuangukiwa ukuta wa nyumba.

Katika tukio la kwanza Mvua ya mawe iliyoambatana na upepo mkali imenyesha katika kijiji cha Nyabehu Kata ya Guta ambapo watoto wawili wamejeruhiwa na mmoja kuvunjika mkono.

Kwa mujibu wa Diwani wa Kata ya Guta MWITA MWANGIERA amebainisha kuwa Mvua imenyesha kwa zaidi ya saa 1 na kusababisha maafa kijijini hapo.

Comments are closed.