MVUTANO WA DIGITALI WAMALIZIKA KENYA

MVUTANO WA DIGITALI WAMALIZIKA KENYA

Like
204
0
Thursday, 05 March 2015
Global News

MVUTANO kati ya Serikali ya Kenya na vyombo vya habari kuhusu kuhamia mfumo wa Digitali kutoka Analogia ambao umesababisha Vituo vinne vikubwa vya Televisheni nchini humo kutorusha matangazo hivi sasa umeisha.

Vituo hivyo mfumo wake wa Analogia ulizimwa,vitaanza kurusha matangazo yake tena.

Makubaliano hayo yamefikiwa March 03 mwaka huu kati ya Serikali na Vituo hivyo vikubwa vya Televisheni nchini Kenya NTV, QTV, KTN na Citizen TV ambavyo vimekubaliwa kurusha matangazo yao jijini Nairobi chini ya Mtandao wa Africa Digital Networks -ADN.

Comments are closed.