WAKATI Leo ni kilele cha siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari, katibu wa baraza la habari Tanzania MCT-KAJUBI MUKAJANGA amesema kuwa uwepo wa vikwazo mbalimbali katika uhuru wa vyombo vya habari ikiwemo uingiliwaj wa urushwaji wa matangazo ya bunge moja kwa moja unaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa urudishwaji nyuma wa mafanikio yaliopatikana katika tasnia ya habari nchini.
Akizungumza na Efm Mukajanga amesema kuwa wadau wa habari wakiwemo waandishi wa Habari na serikali wana kazi kubwa ya kulinda mafanikio yaliopatikana katika tasnia hiyo kwa faida ya nchi hasa kwa kuhimiza sera bora na utawala wa sheria.
Ameongeza kuwa inapaswa kila idara na taasisi kutambua majukumu yake na kuacha kuingilia baadhi ya kazi na majukumu ya taasisi au chombo flani.