MWILI WA MAKAIDI KUAGWA LEO

MWILI WA MAKAIDI KUAGWA LEO

Like
210
0
Tuesday, 20 October 2015
Local News

MWILI wa aliyekuwa Mwenyekiti Mwenza wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) Dokta Emmanueli Makaidi unatarajiwa kuagwa leo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

 

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam jana mtoto wa marehemu Mhandisi Emmanueli Makaidi amesema mwili huo baada ya kutoka Masasi ulipelekwa Hospitali ya Jeshi Lugalo ambapo jana jioni ilifanyika ibada fupi nyumbani kwa marehemu.

 

Shughuli ya kuuaga mwili wa marehemu itahudhuriwa na  viongozi mbalimbali wa kisiasa na serikali na kufuatiwa na mazishi yake katika makaburi ya Sinza Jijini Dar es salaam.

Comments are closed.