NAHODHA WA BAFANABAFANA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUPIGWA RISASI

NAHODHA WA BAFANABAFANA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUPIGWA RISASI

Like
436
0
Monday, 27 October 2014
Slider

Nahodha ambaye pia ni golikipa wa timu ya soka ya taifa la Afrika kusini Senzo Meyiwa amefariki dunia baada ya kupigwa risasi.

Jeshi la polisi la nchi hiyo limesema.

bafana

Senzo Meyiwa Ezi ya uhai wake

Tukio hilo limeripotiwa kutokea katika nyumba ya mpenzi wake iliyopo katika mji wa Vosloorus kusini mwa Johannesburg.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 aliichezea klabu ya Orlando Pirates na alicheza mechi nne zilizopita za timu yake ya taifa katika mechi za kufuzu za fainali ya mataifa ya Afrika.

Jumamosi alikuwepo katika tukio la timu yake pindi waliposonga mbele katika nusu fainali ya ligi ya Afrika kusini.

Katika maelezo yake Jeshi la polisi la afrika kusini limesema kwamba Meyiwa ameripotiwa kufariki wakati akiwasili hospitalini.

 

Comments are closed.