NDEGE YA MIZIGO YAANGUKA SUDANI KUSINI

NDEGE YA MIZIGO YAANGUKA SUDANI KUSINI

Like
307
0
Wednesday, 04 November 2015
Global News

NDEGE ya  mizigo imeanguka muda mfupi baada ya kuruka kutoka katika uwanja wa ndege nchini Sudan Kusini na kusababisha vifo vya watu takriban  41 waliokuwemo ndani ya ndege hiyo pamoja na waliokuwa maeneo iliko tokea ajali hiyo.

 

Msemaji wa ofisi ya rais Ateny Wek Ateny amesema muhudumu mmoja na mtoto wamenusurika katika ajali hiyo.

 

Mwandishi wa shirika la habari wa AP aliyekuwa karibu na eneo la tukio amesema alishuhudia mabaki ya ndege hiyo yalionekana yametawanyika upande wa mashariki mwa Mto Nile.

Comments are closed.