NEC YAENDELEA KUTOA MATOKEO NGAZI YA URAIS

NEC YAENDELEA KUTOA MATOKEO NGAZI YA URAIS

Like
208
0
Tuesday, 27 October 2015
Local News

TUME ya Taifa ya Uchaguzi-NEC-imeendelea kutoa matokeo kwa ngazi ya Urais kutoka majimbo mbalimbali yaliyokamilisha Zoezi la kuhesabu kura zilizopigwa katika Uchaguzi mkuu uliofanyika oktoba 25 mwaka huu.

Awali akizungumza kabla ya kutangazwa kwa matokeo hayo leo katika ukumbi wa mikutano wa mwalimu Nyerere Jijini Dar es salaam mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji mstaafu Damian Lubuva amewataka wananchi kuondoa wasiwasi kwani Tume imejipanga vyema kuhakikisha kila matokeo yanayopatikana inayatangaza.

Leo ni siku ya pili tangu kukamilika kwa Zoezi la upigaji kura ambapo kwa sasa Zoezi la kutangaza matokeo ya nafasi mbalimbali linaendelea kwa nchi nzima.

Comments are closed.